Tuesday, January 13, 2009

Mapambano dhidi ya ujinga!!


Mapambano dhidi ya adui ujinga yashika kasi! Shirika la Elimu Kibaha limeanzisha shule ya sekondari maalum kwa wasichana. Shule hii kwa sasa ni ya kutwa na inaitwa "Kibaha Girls' Sec. School. Shule nyingine za sekondari zilizo chini ya Shirika la Elimu Kibaha ni Kibaha Sekondari na Tumbi Sekondari. Vile vile kuna chuo cha maendeleo ya wananchi na chuo cha wauguzi. Karibu Shirika la Elimu Kibaha ujionee!

Karibuni kwa maoni

Kuhitimu mbona utamu!!


Safari ni hatua! Katika safari ya kupata elimu, kuna raha yake katika kila kituo muhitimu anapofikia. Pichani ni wafanyakazi mbalimbali katika Shirika la Elimu Kibaha wakifurahia nondo walizozipata kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi. "Watanzania tuna kiu ya kusikia na kujifunza toka kwenu"


Karibuni kwa maoni.