Monday, April 9, 2007

Pozi lake lina mvuto!

Moja ya hazina kubwa ya taifa. Anaonekana kama anasema "ok. nipo tayari nipige picha". Pundamilia huyu ni moja ya vivutio vingi vilivyo katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Crater. Katika karne hii ya sayansi na teknolojia ni muhimu kuvitangaza vivutio hivi. Kama ilivyo habari, biashara pia ni kutangaziana!

3 comments:

Simon Kitururu said...

Pundamilia kapendeza. Lakini sijui kwanini huyu mnyama tulishindwa kumtumia kama punda wa kawaida. Tembo wetu pia Afrika ni kasheshe kumtumia. Waasia kuna baadhi ya wanyama wametushinda kuwafunza kinamna mpaka wakatumika kwa shughuli za kinamna. Lakini labda wetu hawafundikishi.

Christian Bwaya said...

Tanzania inao utajiri mwingi lakini ajabu tunaambiwa masikini wakubwa duniani. Haya ni maajabu.

Anonymous said...

Nashukuru kwa mchango wa mawazo yenu. Kweli hawa watu wa magharibi huwa ni wanafiki wakubwa, hawataki shida zao zifahamike na wanajitahidi kujionesha hawana shida. Mimi niko Marekani kwa sasa katika jiji la Chicago, nimeisha ona ombaomba wazungu wengi na wako mitaani ukipita wanakuomba uwape hela. Wapo wazungu ambao hawawezi kulipia matibabu, ni maskini kweli. Wengine hawawezi kulipia nyumba na umeme, na wengine nyumba zao zina hali ngumu sana kama inavyoonesha picha hii. Lakini wakiandika habari zao huwa hawaongelei matatizo hayo hata kidogo na hujioneha wote ni matajiri na umaskini uko Afrika, Asia na nchi za Amerika ya Kusini. Ni kweli wanatuzidi kwa kiasi kikubwa lakini baadhi yao ni maskini wakubwa ammbao hata huwezi kukuta kwetu.