Chuo Kikuu cha New York kuwa na tawi Tanzania, chatengewa ekari 500!

"Wanakumbukwa kwa kuwa walikuja, wakatenda mema na hatimaye wakaondoka". Mimi na wewe tutakumbukwa kwa yapi?. Ni muda muwali sasa kwa mada jadidi kutekelezwa kwa vitendo na si lelemama. Naamini Tanzania yetu itafanikiwa.
Posted by
MTANZANIA.
at
4:00:00 AM
6 comments:
Je wangapi (wazawa) wataweza kulipa ada za chuo hicho?. Hilo tu.
Ni kweli fido, wangapi wataweza? Kule Misri kuna American University in Cairo, ukiona vijana wanaosoma pale, basi ujue baba au wazazi wao ni tycoons wa namna fulani. Mtu wa kawaida kwake Cairo university!!! na vinginevyo.
Hapa vijana wanalia na asilimia 40 ya tuhela tudogo, je hiyo asilimia 100 ya mahela kibao!!???
Wazo zuri lakini. Wacha walete tu hicho chuo. Tutalima mchicha na kuwasomesha watoto wetu. Yawezekana.
Labda NYU watatoa scolarship! You never know.
na mashuga mami na mashuga dadi watatulipia walalhoi....heh heh.
Habari hii na mimi niliipata kaka nilipokuwa huko mwanzoni mwa mwaka huu. Ni kweli kabisa nadhani itatusaidia saana walalahoi tupate elimu ya kizungu nyumbani. Si unakumbuka kile chuo cha kitapeli cha Waldolf kililamba pesa na kutokomea.
Charahani!
Hawa jamaa wa NYU inaonekana wako makini. Tusuburi, tutayaona. Tusiombe yatokee yale ya Waldolf.
Post a Comment