Monday, October 16, 2023

Nimerejea!

Baada ya kimya cha muda naomba kuwajulisheni kuwa nimerejea tena wakuu

Sunday, November 20, 2011

Tabasamu na urafiki!



Karibuni kwa maoni

Mashaka na urafiki wa mashaka!



Karibuni kwa maoni

Friday, February 13, 2009

Robertine!


Karibuni kwa maoni

Thursday, February 12, 2009

Naogopa mkorogo!!

Moja kati ya magwiji wa muziki wa Kikongo. Huyu si mwingine ila ni Papa Wemba a.k.a naogopa mkorogo.

Karibuni kwa maoni

Monday, February 9, 2009

Korogwe Chuo cha Ualimu!!

Hapa ni kwenye lango kuu kuingia chuoni.

Ni chuo kilichopo mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe. Ni moja kati ya vyuo vikongwe kabisa hapa nchini ambapo walimu wetu wengi wamepita na kujizolea "teaching Pedagogy". Ni mahala pazuri pa kutembelea!

Karibuni kwa maoni

Tuesday, February 3, 2009

Tuupige vita ukimwi!!

Ndivyo wanavyoonekana kujadili. Hawa ni baadhi ya vijana waliopo shule za sekondari. Hapa ni Silver Sand Camping & Site ulipofanyika mkutano mkuu wa kitaifa wa kutimiza miaka 10 wa shirika lisilo la serikali la Femina Hip.

Tuesday, January 13, 2009

Mapambano dhidi ya ujinga!!


Mapambano dhidi ya adui ujinga yashika kasi! Shirika la Elimu Kibaha limeanzisha shule ya sekondari maalum kwa wasichana. Shule hii kwa sasa ni ya kutwa na inaitwa "Kibaha Girls' Sec. School. Shule nyingine za sekondari zilizo chini ya Shirika la Elimu Kibaha ni Kibaha Sekondari na Tumbi Sekondari. Vile vile kuna chuo cha maendeleo ya wananchi na chuo cha wauguzi. Karibu Shirika la Elimu Kibaha ujionee!

Karibuni kwa maoni

Kuhitimu mbona utamu!!


Safari ni hatua! Katika safari ya kupata elimu, kuna raha yake katika kila kituo muhitimu anapofikia. Pichani ni wafanyakazi mbalimbali katika Shirika la Elimu Kibaha wakifurahia nondo walizozipata kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi. "Watanzania tuna kiu ya kusikia na kujifunza toka kwenu"


Karibuni kwa maoni.

Thursday, October 30, 2008

Nimerejea!

Baada ya ukimya wa muda mrefu naomba kuwajulisheni kwamba nimerejea na kwa sasa nina-blogu tokea Kibaha mkoani Pwani. Huku kwa sasa ni mvua tu kwenda mbele. Nitakuwa nikikujulisheni mengi tokea huku.

Thursday, May 10, 2007

Kama ni urafiki mhh! "hii too much".




Kwa jamii yetu mnyama mbwa anafugwa kwa madhumuni ya kusaidia ulinzi. Ila katika jamii nyingine mnyama huyu ni rafiki mkubwa wa binadamu na anapewa heshima zote za rafiki wa kweli. Kudhihirisha hilo ni kosa kubwa kwa wenzetu hawa kumtaja mnyama huyu kwa kutumia pronoun "it". Huwakilishwa na pronoun sawia kabisa na binadamu. Mathalani mbwa dume ni "he" na mbwa jike ni "she". Huo ni mfano mmoja tu wa heshima apewayo mnyama mbwa. Naamini ipo mingi.

Saturday, May 5, 2007

Ujumbe!

Serikali ya Tanzania imedhamiria kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini. Hapa ni siku ujumbe wa Tanzania ulipokitembelea chuo kikuu cha New York kwa ajili hiyo. Timu iliongozwa na Mh. Jumanne Maghembe (Waziri wa maliasili na utalii-wa tatu toka shoto). Pia alikuwepo balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mh. Mahiga-wa nne toka kulia.

Wednesday, May 2, 2007

Hivi kumbe KIMWI chamtoto kwa MALARIA!


Tarehe 25/4 ilikuwa siku ya malaria. Kama ilivyo kwa malaria kuna siku ya UKIMWI pia. Inasikitisha kwamba nguvu nyingi zinatumika katika kupambana na UKIMWI huku malaria ikishika kasi katika kusababisha vifo vingi kuliko UKIMWI. Kwa ujumla inasikitisha na kusononesha kusikia kwamba MALARIA bado ni namba one killer desease hapa Tanzania. Sanjari na hilo karibu zaidi ya 80% ya wagonjwa wanasumbuliwa na malaria huku wengi wao wakiwa watoto na akina mama wajawazito. Nini kifanyike maana malaria inasababisha vifo vingi?

Saturday, April 28, 2007

Kitu hicho!

Ama hakika Teknolojia inakua kila uchao! Hiki kifaa sijui kinaendaje. Wasiwasi wangu ni pale tu kitakapokwaruzwa kama si kugongwa. "weekend njema".

Inawezakana matunda yameanza!


Ziara ya Shaikh Saud bin Saqral Al Qasimi ambaye ni Naibu mtawala wa Ras al Khaiman inaweza ikafungua milango ktk suala zima la uwekezaji hapa nchini Tanzania. Ras Al Khaiman ni miongoni mwa nchi 7 zinazounda muungano wa EMIRATES. Kiuchumi jumuiya ya EMIRATES wamepiga hatua. Ni vema basi viongozi wetu wajifunze mengi toka kwa kiongozi huyo ili kuinua na hatimaye kukuza uchumi wa nchi yetu. Pengine ziara hii ni mojawapo ya matunda ya ziara za viongozi.