Friday, February 23, 2007

Kinyang'anyiro cha Urais wa Marekani 2008, Obama kufurukuta?


Seneta Barack Husein Obama moja ya wanaotajwa kumrithi Bush akitangaza azma yake ya kuwania nafasi hiyo.
Ni uchaguzi unaovuta hisia si tu za wamarekani bali pia watu wa mataifa mbalimbali duniani kote. Kinadharia inaonekana kama vile Democratic watashinda uchaguzi huo kwa vile ndicho kinacholidhibiti baraza la Congress. Lakini pia suala la vita nchini Iraq limekipunguzia umaarufu chama cha Republican. Ndani ya Democratic kuna pilikapilika za kuwania kuteuliwa kwa ajili ya kukiwakilisha chama katika uchaguzi huo. Wanaotajwa sana ni Seneta Barack Obama na Hilary Clinton mke wa Bill Clinton. Je uraisi wa Marekani kuendelea kuwa mikononi mwa familia mbili yaani familia ya Bush na Clinton iwapo Hilary atapitishwa? Ni swali linalotokana na baadhi ya vikwazo anavyowekewa Barack Obama. Baadhi ya watu wanalifananisha jina la Obama kama Osama na pia Husein kama lile la Saddam. Wengine wanaenda mbali zaidi ya kwamba kwa vile yeye ni mweusi asitegemee kitu japo watu wanamkubali. Zaidi ya hayo Barack Obama anasemekana alipata kusoma nchini Afghanistan na kwa maana hiyo wanamuona kama mtu anayeweza kuimarisha urafiki kati ya Marekani na nchi za kiarabu. Kipyenga ndio hivyo kimelia na sisi yetu macho. Nani kumrithi Bush? Mweusi au mweupe? Tusubiri!!

4 comments:

Anonymous said...

Makubwa! Mbona anaonekana kachoka. Huyo atapigwa chini tu.

Unknown said...

kimojawapo kati vitu ambavyo jamii za watu weupe duniani zimefanikiwa ni kuwa katika nafasi ya kuamua viwango.kwa viwango vyao Obama ni mweusi,na yeye mwenyewe na watu wengine duniani wanakubali hivyo.ukweli ni kwamba Obama ni nusu mweupe na nusu mweusi.maelezo yake katika majadiliano na mihadhara mbalimbali ni mazuri.naamini ana nafasi ya kushinda,hata hivyo mambo ya siasa mpaka ukiweka kibindoni ndio unakuwa na uhakika!nadhani nchi aliyosoma ni Indonesia na sio Afghanistan.

Anonymous said...

Sensa inaonyesha ya kwamba weupe ni wengi kuliko weusi. Kwa maana hiyo hata akipitishwa na chama atakuwa na kazi ya ziada. Vingenevyo Republica wataitumia hiyo nafasi kutetea kiti kwa kubeba kura zote za weupe.

Patakuwa patamu kama Demokratiki atasimama huyo Obama Osama na Republica akasimamishwa Kondoriza a.k.a Migiro

Simon Kitururu said...

Eti inasemekana mweupe akiwa na tone moja la damu ya mtu mweusi yeye sio mweupe tena.Akina Mariah Carrey nao wanatambulika kama weusi kitu ambacho mimi naona kama ni mazingaombwe. Lakini Tiger Woods anashindwa kukubaliana nahili. Huwa anajaribu sana kutetea mchanganyiko wake hata kwakuweka vipimo vya kihesabu kuhusu mchanganyiko wake. Lakini ukifuatilia haya maswala ya race yanashangaza sana. Lakini Obama hata asiposhinda , nafikiri ni kitu kizuri kuwa anawazoelesha watu kuwa inawezekana. Wote akina Condalisa na Collin Powell nafikiri wamekuwa kielelezo kizuri katika jamii ya watu weusi ingawa sikubaliani nao baadhi ya mitazamo yao.Watu weusi tunahitaji vielelezo , vionyeshavyo kuwa inawezekana.