Wednesday, May 2, 2007

Hivi kumbe KIMWI chamtoto kwa MALARIA!


Tarehe 25/4 ilikuwa siku ya malaria. Kama ilivyo kwa malaria kuna siku ya UKIMWI pia. Inasikitisha kwamba nguvu nyingi zinatumika katika kupambana na UKIMWI huku malaria ikishika kasi katika kusababisha vifo vingi kuliko UKIMWI. Kwa ujumla inasikitisha na kusononesha kusikia kwamba MALARIA bado ni namba one killer desease hapa Tanzania. Sanjari na hilo karibu zaidi ya 80% ya wagonjwa wanasumbuliwa na malaria huku wengi wao wakiwa watoto na akina mama wajawazito. Nini kifanyike maana malaria inasababisha vifo vingi?

4 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Malaria imeua zaidi kuliko 'ngoma' na inaendelea kuua kila kukicha.Ila na hili gonjwa Ukimwi limekaa pabaya kama alivyosema mzee ruksa.

Simon Kitururu said...

Inasikitisha sana!Halafu unajua tena baadhi ya wataalamu wanasema kama umewahi kuugua malaria basi lazima kuna
baadhi ya vidudu vipo tu ndani yako hata kama huumwi.Basi kutokana nahilo nchi kadhaa zinatolea nje mchango wa damu kutoka kwa yeyote aliyewahi kuugua huu ugonjwa.

Lakini ukikatiza mitaa uliyoizoe bongo, karibu kila mtaa utaambiwa kuna mtu kaanza na mdudu pia.

MTANZANIA. said...

@Ndabagoye! Kusema kweli malaria inaua ila nakubaliana na ww ya kwamba "gonjwa limekaa pabaya".


Kitururu umeniogopesha!!!!. Kwa maana hiyo basi wabongo wote tuna malaria. Naamini hakuna ambaye hakuwahi ugua malaria tokea azaliwe. Kazi kwelikweli.

Simon Kitururu said...

@Mtanzania:Inatisha kweli Mzee!Hata mimi simjui Mtanzania yeyote aliyeishi Tanzania halafu hajawahi kuugua Malaria