Wednesday, April 18, 2007

Hivi ulifanyalo ndo hasa ulistahili kulifanya!!!


Pichani baba watoto akiwa makini kutoa maelekezo kwa wanawe wanaojaribu kuchora huku mama yao akitazama. Ni njia thabiti ya kuendeleza vipaji.

Kipaji (ability/talent) ni ile hali ambayo kiasili mtu anakuwa na uwezo au mapenzi ya kufanya jambo fulani. Aghalabu vipaji huonekana tangia utotoni. Kila mtoto huwa anaonyesha kile anachokipenda (interest) kwa kujaribu kukifanya mara kwa mara. Kawaida vipaji vinapaswa kuendelezwa na kukuzwa katika mazingira mazuri. Wawajibikaji wakuu kwa hilo ni wazazi au walezi (care givers). Kwa kufanya hivyo watoto watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuyafanya yale wayapendayo. Kama mtoto anaonyesha mapenzi katika kusakata kabumbu basi ni vema aipate elimu yake katika shule zenye mchepuo wa michezo. Sina uhakika kama hili nilifanyalo ndio hasa nililokuwa nikilipenda tangu utotoni. (sikufuru). Lakini nakumbuka nilikuwa napenda sana kuwa muuza duka na nilikuwa nikiwasumbua sana wazazi wangu kwa hilo. Kwa undani huenda kipaji changu kilikuwa biashara. Katika nchi zilizoendelea suala hili linazingatiwa sana kwa ushirikiano wa wazazi na serikali. Kwa kuhitimisha, napenda nikuulize swali dogo mpenzi msomaji, Je hiyo shughuli yako uifanyayo au hiyo kozi unayosoma ni ile hasa ambayo inaendana na kipaji chako?

3 comments:

Simon Kitururu said...

Mimi nafikiri mara nyingi sisi Waafrika hujali zaidi ni wapi kuna maslahi. Na hili ni wazazi hulijenga kwa njia nyingi tu vichwani mwa watoto. Nilipomuuliza Baba yngu ni nini Babu alitaka afanye,akasema babu alimsisitizia achukue Ualimu au Uchungaji. Kisa ilikuwa hadhi ya ualimu na uchungaji ilikuwa iko juu sana.Na ilimchukua muda babu kuamini kuwa Mzee anafaya poa katika anga aliojichagulia.

Tukirudi katika kizazi changu, ilikuwa kawaida kabisa wakati wa kuchagua kombi mtu kuchagua usikiacho kuwa kinamaslahi. Hivyo naamini asilimia kubwa ya Watanzania hawafanyi walilokuwa wakilipenda tokea udogoni.Hatuna tamaduni zituwezeshazo kuendeleza vipaji vya watoto bila kuingiza ujuaji wetu wa nini tunafikiria watoto wafanye.Mara nyingine wazazi huchagulia watoto shughuli ilimradi tu kujifurahisha wao na sio kwa manufaa ya mtoto, au kwa furaha ya watoto.

Lakini nafikiri umasikini nao unachangia sana.Kutokana na umaskini wengi wetu hatuna eneo kubwa la kuchagua.Ni rahisi hata mtoto kutishika kufanya apendacho kama kinapingana na matakwa ya wazazi kwa kuogopa kukwama halafu kulaumiwa kuwa, sisi tulikuambia, sasa kazi kwako.Hili hasa husababishwa na mtoto kumtegemea mzazi ki maslahi.

Mikundu Matako Makalio Manundu said...

Ahsante sana kwa falsafa zako, ukichoka na falsfa tafadhali pitia kwa Mzee Mikundu ukajiliwaze kidogo, hakuna zaidi ya picha za mikundu tuu:

http://mikundu.blogspot.com/

Anonymous said...

tunaomba mchango wako hapa https://www2.blogger.com/comment.g?blogID=17229004&postID=2228567355941212162