Wednesday, April 4, 2007

Nyota yake iling'ara tokea akiwa bado kinda.

Vipaji (talents) mara nyingi huonekana tokea utotoni. Franco akiwa na miaka 7 alifanikiwa kutengeneza gitaa kwa kutumia lililokuwa kopo la bati la kuhifadhia mafuta ya kupikia. Alilitumia gitaa hilo kutoa burudani kwenye mechi za kandanda. Alifanikiwa kupata gitaa halisi alipokuwa na umri wa miaka 11. Wakati huo alikuwa kama mpiga gitaa wa muda tu katika studio ya Loningisa iliyokuwa ikimilikiwa na Wagiriki huko nchini Zaire. Kipindi hicho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa chini ya utawala wa Ubelgiji. Mwaka 1956, Makiadi alifanikiwa rasmi kuanzisha bendi ya OK Jazz ambayo baadaye ilikuja kujulikana kama TPOK Jazz. Aliongeza "TP=Tout Puissant" yenye maana ya "wote wana nguvu". Tizama moja ya kazi zake hapa.

5 comments:

west vibe said...

I like his song though I don't understand the language. You have to teach me the language.
Cool job!

Anonymous said...

Mtu wangu!
Hata mm umenigusa kwa historia ya huyu gwiji. Kimsingi "alikubalika"

Evarist Chahali said...

Nashukuru kwa kutembelea nyumba yangu,nami nimebahatika kutembelea hapa kwako.Nimepapenda sana na nitakuwa natembelea mara kwa mara.

Simon Kitururu said...

Mtanzania, huyu Mzee mimi nimemkubali.Sina ujanja

Anonymous said...

hilo gwiji