Thursday, January 18, 2007

Kandanda ni kipaji na elimu pia.

Pichani Mwl. Merchedes Method (katikati) aliye chuo kikuu cha Wisconsin akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa kocha wa chuo (hayupo pichani) wakati wa mapumziko. Katika mechi hiyo Wisc. walishinda 2-0 huku yeye akiwa kapachika kimiani bao moja.
Wakati dunia hivi sasa inashuhudia maendeleo makubwa ya Sayansi na Teknolojia katika kila nyanja, soka la Tanzania limeendelea kutawaliwa na vibweka vinavyoashiria imani kali za kishirikina kama inavyokuwa wakati wa mpambano wa vigogo vya soka nchini Simba na Yanga.Umefika wakati sasa kuachana na imani hizo na kuwekeza katika rasilimali watu ili kuinua kiwango cha kabumbu la bongo.Tanzania imejaliwa vipaji vingi vya wachezaji. Mojawapo ya vipaji hivyo ni kijana Merchedes Method (double M) aliye katika chuo kikuu cha Wisconsin nchini Marekani. Licha ya kufundisha kiswahili chuoni hapo,pia amejijengea umaarufu mkubwa katika fani ya mpira wa miguu maarufu kama futibo.Amekuwa gumzo chuoni hapo kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira,kupangua misitu ya mabeki kwa chenga za maudhi na pia kwa mashuti yake mazito.Habari njema kwa Tanzania kwa ujumla ni kwamba kijana huyo pia anahudhuria mafunzo ya ukocha chuoni hapo.Tunamuomba akimaliza muda wake arejee nchini na kuboresha mchezo wa mpira wa miguu.

2 comments:

Anonymous said...

Inawezekana zikawa habari njema kama kweli atarudi bongo.Wengi wamekuwa wakiishia huko huko Unyamwezini kwa kile wanachokiita "green pastures".Jitahidi bwana na angalia umaarufu usikuponze.

Zablon Mgonja said...

Baba kamuaaaaaaaaaaaaaa nimekuaminia