Tuzithamini bidhaa za ndani.
(Pichani; Bidhaa za kigeni ambazo kimsingi tunakula ili tushibe. Mara nyingi vyakula hivi huwa havina ladha nzuri na asilia.)
Binadamu tunatofautiana kwa silka na hulka. Kila mtu ana tabia zake ambazo haiyumkini zaweza kuwa nzuri au mbaya pia. Binafsi naweza sema umaarufu ni moja ya sifa kubwa inayotafutwa kwa nguvu zote na asilia kubwa ya binadamu. Kuna haja gani ya kwenda kulinunua chenza toka Afrika ya Kusini lenye ubora sawa na lile linalotoka Muheza kwa bei ya juu? Hainingii akilini na ndio maana naona kama huo ni utafutaji tu wa umaarufu.
Kwa bidhaa za mashambani Tanzania tumejaliwa (endowed) aina mbalimbali za vyakula vilivyo na ubora wa kutosha.Mathalani kuna machungwa yanaozea mitini huko Muheza,kuna milima kama si vifusi vya mananasi pale Chalinze,kuna ndizi nyingi huko Tukuyu,Mlimba na Bukoba.Viazi pia vipo vya kutosha huko Njombe na Morogoro.Nyanya zinapatikana kwa wingi Iringa na Morogoro.Hiyo ni mifano michache tu.Pamoja na uwingi wa bidhaa bora toka ndani ya nchi, haiyumkini bado kuna hizi zinazoitwa "Shopping centres" mijini zenye kuuza bidhaa za kigeni za mashambani kama vile matunda kutoka nchini Afrika ya Kusini tena kwa bei ya juu. Umefika wakati sasa kwa walaji kubadilika na kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwetu kwamba kila kinachotoka ng'ambo ni bora.Sambamba na hilo kuna haja ya kuboresha mazingira na kukuza soko la bidhaa za ndani kwa minajili ya kuwanusuru wakulima na wazalishaji wa ndani na pia kukuza pato la taifa.Kwa ufupi linahitajika soko madhubuti na mipango endelevu kwa ajili ya bidhaa za ndani.Tusipokuwa makini kuna siku maduka haya makubwa yatatuuzia chapati zilizookwa Afrika ya Kusini na Uarabuni.

2 comments:
We mshikaji mbona umebadilika hivi?Nafikiri ni ww uliyemaliza pale mlimani.Uko wapi kwa sasa?
Ni kweli kabisa unalosema mzee wangu! Haya mavyakula ya akina shprait na kadhalika yanatuzuga mengine ya siku nyiiiiiiiiiiiiiiiiingi hadi basi, mengine yamewekewa viini vya kufanya vitu vikue haraka, mengine kabla hayajamaliza mzunguko wake wa kukua. Matokeo yake watu wanapokula yanasababisha saratani kwani ile sehemu iliyopaswa kukua kwenye mmea inakua kwenye mwili. Loh jamani tuleni vya asili
Post a Comment