Tuesday, January 30, 2007

Ni shule mtindo mmoja bila kujali umekalia kiti au umekaa chini.

Hali inavyokuwa wakati wa muhadhara katika moja ya kumbi za mihadhara chuo kikuu Mlimani.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam pengine ndio taasisi kubwa ya elimu ya juu kuliko taasisi nyingine zote. Si tu ni taasisi kubwa kwa kuwa na muda mrefu tokea kuanzishwa, bali pia ndiyo taasisi pekee inayodahiri idadi kubwa ya wanafunzi kwa ajili ya stashahada, shahada, na shahada za uzamili. Taasisi hii kwa sasa inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwa ni pamoja na uwiano usiokuwa sawia baina ya idadi ya wanafunzi na vitendea kazi kwa ujumla wake. Mathalani kumbi za mihadhara zilizojengwa kwa ajili ya kupokea wanafunzi 400, kwa sasa zinalazimika kutumiwa na wanafunzi zaidi ya 1000. Katika nadharia ya kweli ili mwanafunzi aelewe vizuri kile anachofunzwa anapaswa kuwa katika mazingira mazuri huku akili ikiwa imetulia. Lakini kwa chuo chetu hiki hali ni tofauti maana muda mwingi mwanafunzi anawaza kama kipindi kijacho utapata kiti au utaketi chini tena. Ndio hivyo kwa mazingira hayo hayo watu wanahitimu kila mwaka. Ni wakati sasa kwa uongozi wa chuo kwa kushirikiana na serikali yetu kuyabadili mazingira ya chuo ili kiwe na hadhi ya chuo kikuu. "Elimu ndio ufunguo wa maendeleo".



2 comments:

Anonymous said...

Duh! jamani si wapanue hizo lecture rooms ili kukidhi namba ya wanafunzi.Hapo ni shida tu na hili joto la DSM.

Zablon Mgonja said...

Inaumiza moyo kwa kweli! Mi naona serikali yetu haijui mambo ya kupewa kipaumbele. Hivi kweli ni haki katika zama hizi mhadhara wa chuo kikuu kufanyika watu wakiwa wamekaa chini!

Mi nakumbuka mwaka 2003 nilipokuwa mwanafunzi kwenye moja ya vyumba hivyo vya mihadhara, kuna somo moja lilikuwa llina idadi ya watu 1004 huku chumba kina uwezo wa kubeba watu 460 tu! Halikupatiwa ufumbuzi hadi wanafunzi walipolalamika na kugoma ndio likatatuliwa. Hata hivyo utatuzi wake ulikuwa ni kuumiza wahadhiri kwani ilibidi darasa ligawanywe mara tatu, jambo lililofanya mhadhiri mmoja kuwa na idadi kuuuuuubwa ya vipindi katika juma moja.

Hii ni hatari! Wakati mwingine inaweza kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu kwani mhadhiri anakosa muda wa kujiandaa kutokana na lundo kuuuuuuubwa la kazi!
Nashauri tulijadili hili kw undani.

Mambo haya yapo tofauti. Kuna ule msemo wa MWENYE KUCHA HANA PA KUKUNA NA MWENYE PA KUKUNA HANA KUCHA ZA KUKUNIA, hapa Marekani, idadi kuubwa kabisa ya wanafunzi kwa darasa moja ni 20, na chumba bado kinasalia na nafasi kuuuubwa kabisa ya kupungia hewa.

KAma wapo wengi na wanafundishwa na walimu mmojabasi ujue madarasa yao yanafanyika kwa njia ya mtandao na hawahitaji uwepo wa mwalimu moja kwa moja. Hata kama hatujafikia kiwango cha mitandao na kozi za masafa marefu, basi tujipige pige walau madarasa yawepo na wahadhiri walipwe vizuri ili waongezeke katika taasisi za elimu ya juu.

Mnchi isiyo na elimu bora na endelevu, katu haiwezi kuendelea