Monday, January 22, 2007

Upi muziki wa Tanzania?

Wahenga walinena "kazi na dawa".Ndivyo inavyojidhihirisha katika picha ambapo waafrika mbalimbali waliamua kuifurahia ladha ya taarabu wakati wa sherehe za kuanza muhula wa pili wa masomo hapa NYU. Sipo pichani,ila kabla ya hapo niliwapa shule kidogo namna ya kuicheza na hayo ndo matokeo yake.

Miongoni mwa maswali magumu nilowahi kuulizwa ni hili la kuhusu muziki wa Tanzania.Kwa sababu ilikuwa ni mkusanyiko wa Waafrika mbalimbali na wengi wao walikuwa kutoka Afrika magharib,msema chochote hakuchelewa kuniita na mara baada ya kunitambuza aliniuliza ni upi muziki ambao ni kielelezo cha Tanzania kiasi kwamba ukiusikia tu unajua huu ni kutoka Tanzania? Palikuwa hapatoshi lakini kwa vile nilikuwa na CD za taarabu ikabidi nimwambie ni "taarabu" ili kuepuka aibu ya kuiangusha nchi yangu miongoni mwa macho ya wageni wengine. Basi kutoka kwenye hiyo CD ya East Africa Melody kilipigwa kibao cha "viumbe wazito" na nika-demonstrate namna ya kuicheza taarabu kabla ya hadhira kunyanyuka na kuniunga mkono. Baada ya hizo dondoo chache narudi kwenye mada kuu kwamba upi hasa ndo muziki wa Tanzania? Nashindwa na sijui sawasawa kati ya mduara,taarabu,dansi,bongo flava, n.k ni upi ndo kielelezo cha muziki wa Tanzania. Dunia kwa hivi sasa imekuwa kijiji kimoja na kwa maana hiyo waweza kutumia lugha yoyote ile lakini bado uka-maintain muziki wa asili yako.Mfano halisi ni kundi la Mandinka toka Afrika magharib wana wimbo wao moja wenye maneno mengi ya kiswahili lakini bado ukiusikia unajua kabisa ni kutoka Afrika ya magharibi.Kwa anayejua anisaidie kunijuvya ni upi hasa ndo muziki wa Tanzania?




2 comments:

Anonymous said...

Ungesema dansi na ungetumia msondo (OTTU) katika kuuelezea muziki wa Tanzania.

MTANZANIA. said...

Asante Gurumo kwa wazo lako zuri.Bado sina uhakika kama kweli msondo ndio wanawakilisha aina ya muziki ambao ni utambulisho wa Tanzania.Naendelea kuyatafuta majibu muafaka.