Tuesday, January 30, 2007

Vivutio si kwa ajili ya wageni tu, hata wazalendo tunaweza kuwa watalii.

(Pichani watanzania waishio Moshi walioamua kutembelea vivutio mbalimbali kama bango linavyojionyesha. Picha kwa hisani ya Juma Iddi Issa -wa kwanza toka kushoto.)

Tanzania yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi kama vile mbuga za wanyama, mabonde mazuri ya kuvutia, mlima mrefu wa Kilimanjaro, maziwa na mito mingi karibu kila kona ya nchi. Lakini wageni toka nje ya nchi ndio kwa asilimia kubwa wanaovitembelea vivutio hivyo ikilinganishwa na wazawa. Binafsi naweza sema ni kasumba ambayo wazalendo tumejijengea ya kwamba vivutio hivi ni kwa ajili ya wageni (watalii). Kimsingi si wanaotoka nje tu ndio wanapaswa kuwa watalii bali hata sisi watanzania tunaweza kabisa kuwa watalii kwenye vivutio mbalimbali ndani ya nchi yetu. Cha msingi hapa ni serikali kupunguza viingilio kwa wazawa ili kutoa nafasi kubwa kwa wananchi bila kujali vipato vyao. Ni aibu mtu kutoka Amerika ya kusini au Mashariki ya mbali na kuuetembelea mlima Kilimanjaro ili hali mimi na wewe tuliozaliwa na kukulia Tanzania si tu hatujawahi kuutembelea bali hata historia yake hatuijui vizuri. "Nakupenda Tanzania"

1 comment:

Anonymous said...

Bwana Abou waweza nifahamisha kama hao wakubwa walienda hapo kwa ajili ya semina elekezi au kwa ajili ya kutalii? Maana bongo kila kitu semina elekezi huko Ngurdoto.
Kazi kweli2.