Monday, January 15, 2007

Dhana ya sadaka.

Muongozo wa dini ya kiislam.
Sadaka katika lugha rahisi ni kitu chochote kinachotolewa na mwenyenacho ili kumsaidia asiyekuwa nacho. Kiundani, mtu yoyote anaweza kutoa sadaka bila kujali kama ni tajiri au masikini. Inasemekana sadaka ya masikini ni bora zaidi kuliko sadaka ya tajiri.Sadaka inaweza ikawa chakula,mavazi,fedha n.k. Dini zote zimeweka wazi kwamba sadaka ni siri kiasi kwamba kama umeitoa kwa mkono wa kulia basi hata ule wa kushoto usijue kuwa mkono wa kulia umetoa nini.Kimsingi sadaka sio jambo la kutangaza kwa maana ya kwamba unapoitoa,unakuwa unamtolea Mungu naye anakuona.Kama utaitoa sadaka kwa minajili ya kujipatia umaarufu/ufahari ama hakika haiwezi pata baraka toka kwa Mungu.Maoni yangu ni kwamba sadaka zitolewe kama dini zetu zinavyoelekeza.

3 comments:

Anonymous said...

Swadakta! Ww unatoa lakini au unashauri tu? Umetoa changamoto kwa wenye kutoa sadaka kwa ajili ya misifa! Nimekapenda ka-blog kao.

Anonymous said...

Salim Keep it up blog yako ni nzuri sana endelea kaka swafi

MTANZANIA. said...

Asante anony. wote kwa kunitembelea. Kwa anony wa kwanza sina jibu na siwezi sema kama natoa au sitoi. Majibu anayajua Mungu kama mada inavyojieleza. Kwa anony wa pili nimekupata lakini naungana na Raisi JK kutopenda kusifiwa. Otherwise bado nina safari ndefu.