Tuesday, January 23, 2007

Kama ni koleo, basi liitwe koleo.

(Pichani mwenye batiki ni mke wa mwanaharakati mahiri kutoka Kenya aitwaye Ngugi wa Thiong'o. Wengine ni wanafunzi wa NYU kutoka nchini Tanzania na Kenya.)
Kwa umri nilionao nimepata kuyasikia maneno mbalimbali yakiwa na maana tofauti.Mengi ya maneno yasiyotamkika mbele ya hadhira nilikuwa nikiyasikia tu toka kwa wale wa rika langu bila kujali jinsia. Hakuna anayeweza kubisha kwamba wanapokutana watu wa rika moja si muda wote huwa wanakuwa serious, kuna wakati hali hubadilika na maneno mbadala hutumika ili kuchagiza story. (siwezi yataja hapa). Baada ya utangulizi huo,napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mke wa Ngugi wa Thiong'o anayejulikana kama Nyeri wa Ngugi. Bila shaka unakumbuka mkasa uliowapata yeye na mme wake walipoitembelea Kenya mwaka 2005.Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, mama huyu mbele ya kadamnasi iliyokuwa imekusanyika katika ukumbi wa Silver Centre hapa New York University alibainisha ukweli na kwa kuyatumia maneno halisi kwamba walipovamiwa na majambazi licha ya kuporwa pia walitenganishwa vyumba na hatimaye wakamuingilia kwa nguvu (kumbaka). Akiendelea kufafanua anasema alikuwa anahofia sana kuambukizwa ukimwi na si vinginevyo.Lakini kwa taratibu za wanawake wa Kenya na Afrika kwa ujumla ni nadra sana kwa mtu aliyeolewa kusema amebakwa. Yawezekana ni kwa kuogopa talaka au aibu (mimi sijui). Sasa kutokana na hii tabia ndio maana ninadiriki kutoa shukrani kwa mama huyu aliye na umri zaidi ya mama yangu kwa kuwa muwazi na kuyatamka hadharani maswahibu yaliyompata. Hii ni changamoto kwa wanawake hasa walio kwenye ndoa ya kwamba "koleo ni lazima waliite koleo"

3 comments:

Zablon Mgonja said...

Mara zote ukweli huwa unakuwa mgumu kusemwa hasa unapoluwa ni ule unaoumiza mtu fulani. Hata hivyo kutokuusema ukweli huo hakuuondolei sifa yake ya kuwa ukweli, ila tunapoanza kutafuta maneno meeeeeeengi mbadala huenda hata ukapotoka na ukawa uongo.
Huyu mama ameonesha ujasiri wa hali ya juu mno kwani ni wengi wamefanyiwa vitendo vya kinyama namna hiyo na hawavitaji matokeo yake vitendo hivi vinaendelea kutokea.
Nadhani namna nzuri ya kuvipinga ni kuviweka wazi

MTANZANIA. said...

Swadakta Kilimanjaro! Nimekupata na nashukuru sana kwa kunitembelea. Cha msingi hapa ni kwamba akina mama wasilipe nafasi suala la aibu katika mchakato mzima wa kuuondoa udhalimu wanaofanyiwa wanawake.

shamim a.k.a Zeze said...

habari mtz

website yako nzuri imependa ulivyomix vitu unagonga kila idara watoto wa mjini wanasema

nimependa hiyo picha ya mama ngugi kwani kapendeza saana natamani niibe niiweke kwenye fashion...RUKSA????

KAZI NZURI...kaza buti