Thursday, February 1, 2007

Rada, moto uliozimika na kulipuka tena.

Mh. JK Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifafanua jambo kuhusu mustakabali wa Taifa letu.

Kwa kile kilichoelezwa kuwa ni harakati za kiusalama, serikali ya Tanzania mnamo mwaka 2002 ilitumia karibu Tshs bilioni 50 kwa ajili ya manunuzi ya Rada toka kwa serikali ya Uingereza kupitia shirika la BAE System. Mengi yalisemwa na watanzania wakati wa mchakato mzima wa suala la ununuzi wa rada na hatimaye yakasahaulika hadi mwaka huu baada ya wabunge wa Uingereza kuihoji serikali yao kwa kile kinachoonekana kuwa haikutenda haki kuiuzia Tanzania chombo hicho ambacho si cha kisasa tena kwa bei ya juu. Hivi sasa suala hilo kwa upande wa Uingereza limeachiwa Kitengo cha Kupambana na Makosa ya Ulaghai (SFO) ili kuchunguza madai kuwa kampuni ya BAE Systerm iliiuza rada hiyo kwa bei ya juu tofauti na bei halisi na pia kama ilitoa kamisheni ya sh. bilioni 12 kwa mtu aliyefanikisha ununuzi huo. Wakati hali ikiwa hivyo huko Uingereza, kwa upande wa Tanzania tayari yaliishafanyika maandamano kulaani ununuzi wa chombo hicho. Serikali imesisitiza kwamba inasubiri ripoti kutoka Uingereza ili kujua kama kuna watanzania waliohusika katika kashfa hiyo. Katika kulizungumzia sakata hilo serikali imesisitiza iwapo uchunguzi utabaini ya kwamba Tanzania ilidhulumiwa, kuna uwezekano mkubwa itatuma maombi kwa Serikali ya Uingereza ili kudai fedha zilizozidi. "Rada moto uliozimika na kulipuka upya".

3 comments:

Simon Kitururu said...

Mtanzania asante kwa kunitembelea.Lakini nashukuru kukutana na mtu aonaye mambo kama mimi.Fikiria heti mpaka bunge la Uingereza ndio linashtukia kua maswala sio safi katika dili walioingia watuwakilishao.Tuna kazi!

MTANZANIA. said...

Kitururu jisikie uko nyumbani. Ni kweli suala hili linasikitisha ukizingatia ya kwamba kifaa chenyewe ni cha kizamani na pia kilinunuliwa maradufu ya bei yake. Yetu macho na tuisubiri hiyo ripoti. Kusema kweli ni kazi kwelikweli.

John Mwaipopo said...

Mtanzania asante kwa kunisabahi pale nyumbani kwangu. Humu mwako kunamambo ati. Kuna fikra pevu na jadidi. Hapana shaka nitakuwa (nikipata fursa) natembelea mara kwa mara mosi kwako nitakuwa najikumbushia New Jersey mwaka jana (Nilikuwa Paterson) pili kujua yaliyojiri fikirani mwako. Asante.