Saturday, February 10, 2007

Baada ya pindua pindua Dar, Bonde la ufa-RVF laitikisa Arusha.

"Imepimwa hii na kuthibitishwa na mganga kuwa haina RVF". Nahisi ndivyo asemavyo huyu muuzaji wa duka la nyama jijini Dar es Salaam.


Ni ugonjwa ambao huikumba mifugo hususan iliyo katika bonde la ufa na hii ndio sababu hasa ya kupewa jina hili. Binafsi natoka katika jamii ya wafugaji na ugonjwa ambao niliwahi kushuhudia madhara yake kwa binadamu ni kimeta. Nilishuhudia watoto wawili wa familia moja wakipoteza maisha na watu wengine watano wa familia hiyohiyo wakiponea chupuchupu kupoteza maisha kwa kula nyama ya ng'ombe aliyekuwa na kimeta. Kwa ujumla magonjwa haya ya mifugo aghalabu huwa mwiba na tishio siyo tu kwa maisha bali hata biashara. Kwa kawaida watu wengi katika kipindi hiki huwa wanakuwa makini katika kutumia mazao yatokanayo na mifugo. Lakini kuna wengine wachache ama kwa kutoelewa madhara yake au kwa kufanya makusudi hujikuta wakiathirika vibaya na kupoteza maisha kwa kuyatumia mazao ya mifugo athirika. Tayari serikali imeisha toa tamko kupitia mawaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa na yule wa Maendeleo ya Mifugo Mh. Anthony Diallo wakiwatahadharisha wananchi kuwa waangalifu wakati wa kula nyama na mazao yote yatokanayo na ng’ombe, mbuzi, nguruwe na kondoo. Ugonjwa huu wa bonde la ufa umejikita Arusha ukitokea nchini Kenya. Jambo la msingi hapa kujiuliza ni je huko vijijini ambako ndiko hasa kwenye wafugaji wengi kuna wataalamu wa mifugo wa kutosha na kama wapo wana vitendea kazi vya uhakika? Sijui maana kijijini kwangu mganga wa mifugo ni moja na anahudumia zaidi ya vijiji vitatu. Zemarcopolo nipo kwenye anga zako, tujadiliane.

6 comments:

Unknown said...

kuna njia kadhaa za kujikinga na RVF;chanjo ya mifugo,chanjo ya watu(bado haiko madukani kwa matumizi ya umma),kujikinga na mbu(vector) nk.kwa nchi kama tanzania pamoja na kuwa na wataalamu wachache lakini inawezekana kuwa na programme ya chanjo kwa wanyama katika maeneo ya epizootics(epidemics among animals).hata hivyo ninaamini kuwa kitu kitakachosaidia kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na RVF kwa kiwango kikubwa katika mazingira kama ya nchi yetu ni elimu juu ya dalili za ugonjwa huu na kusisitiza watu katika jamii za wafugaji kutoa taarifa mapema wanapoona dalili kama hizo.idara ya mifugo nayo inaweza kushiriki kwa kutoa elimu ya dalili kwa wanyama na serikali za vijiji zinaweza kusimamia kuwa wanyama wote waliokufa kwa dalili hizo wanachomwa(sio kufukiwa,kuna wafukuaji!)haya yote yanawezekana iwapo tunaamua,mbona kila kona vijijini na mijini wanajua kuwa sasa hivi nchi inacheza mziki wa nguvu mpya,ari mpya na kasi mpya?jitihada zinazotumika kuwafahamisha "falsafa" hii zikienda sambamba na kuwafamisha juu ya magonjwa kama RVF tutapunguza idadi ya vifo kwa kiwango kikubwa.

MTANZANIA. said...

Naam!
Zemarcopolo umenifungua akili kwa hili.Nililijua mapema na ndio maana nikasema nipo kwenye anga zako. Nilisahau kabisa hili suala la fukuafukua. Ni kweli baadhi ya wafugaji huwa wanafukua mizoga hata kama itakuwa imewekewe sumu, jambo ambalo ni hatari zaidi.

Hii nayo inakuna! ni sahihi kabisa kama nguvu iliyotumika kuitangaza falsafa ya ari,nguvu na kasi mpya ikitumika kuwaelimisha wanachi hususani wafugaji juu ya magonjwa ya mifugo na athari zake,bila shaka madhara yake yatapungua.
Lkn je ni nani wa kulitangaza na kulisimamia hili?

Unknown said...

mtanzania,wakati wa uchaguzi mkuu kuna watu walijaza mafuta kwenye magari wakatembea nchi nzima kuwaomba wananchi wawape jukumu la kusimamia uendeshaji wa shughuli za umma.hao ndio wanapaswa kulitangaza na kulisimamia hili.wasipofanya hivyo wataadhibiwa,hata kama sio leo duniani basi kesho akhera.

Anonymous said...

Wabongo si lazima tule nyama ya ng'ombe au mbuzi. Tuchangamkie kuku, samaki n.k hadi hapo gonjwa litakapoisha.

Unknown said...

mkemia,ulichosema kinatofautiana na ugonjwa wa RVF.ugonjwa huu hauambukizwi kwa kula nyama tu bali hata kwa kugusa majimaji waliyotoka kwa mnyama aliyeathirika.pia mbu wanaweza kuambukiza kama ilivyo kwa maralia.njia nyingine ni kwa kupumua vumbi lililo na mayai ya vijidudu vya RVF,kuna wanasayansi waliopata ugonjwa huu maabara kwa kupumua aerosol iliyo na vijidudu!

Zablon Mgonja said...

Ni muhimu kwa kweli kuwaelimisha watu juu ya namna ya kujiepusha na Ugonjwa huu. MTZ na Ze Marcopolo mmenikumbusha kisa cha kusikitisha, rafiki yangu mmoja alimpoteza mama yake na wadogo zake wawili kutokana na ugonjwa wa KIMETA.

Mambo haya hata hivyo yanaepukika serikali yetu itayapa kipaumbele na si kupiga kelele tu bila kutoa suluhisho la kweli