Saturday, February 10, 2007

Tunakuamkua Abraham Lincoln!


Tukiwa katika makumbusho ya Rais wa 16 wa Marekani Bw. Abraham Lincoln jijini Washington D.C.
George Washington (1789-1797) ndio mtu wa kwanza kula kiapo cha kuwa raisi wa Marekani akiongoza mlolongo wa watu 43. Miongoni mwa watu 43, kuna ambao kamwe hawatasahaulika kwa namna walivyoliongoza vyema taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi na kidola. Majina kama Abraham Lincoln (1861-1865), Theodore Roosevelt (1901-1909), John Kenedy (1961-1963) n.k ni miongoni mwa waliopata mafanikio makubwa katika nafasi hiyo ya uraisi. Kama ilivyo kwa msemo wa kiswahili "vizuri havidumu" Lincoln pamoja na kuwa kiongozi makini aliuwawa kwa kupigwa risasi na mtu aliyejulikana kwa jina la John Wilkes Booth. Hiyo ilikuwa Aprili, 14 1865 baada ya baadhi ya watu kutoridhishwa na sera zake za kuutokomeza ubaguzi na kuwatetea weusi ili kuleta usawa miongoni mwa raia aliokuwa akiwaongoza. Huyo ndio marehemu Lincoln, Raisi wa 16 wa Marekani 1861-1865.

5 comments:

Anonymous said...

Wapi Reegan,Roosevelt, Monroe, n.k

mwandani said...

yaani walimuua kwa sababu alitetea kutokomeza ubaguzi!duniani kuna watu

Simon Kitururu said...

@mwandani. binadamu tunamambo!

MTANZANIA. said...

Mwandani!
Ndivyo historia inavyo-onyesha. Mi nakubaliana na Kitururu ya kwamba bin-adam tuna mambo. Vile2 vizuri huwa havidumu.

Anonymous said...

Kuna msemo Bongo: 'Ukitaka ugomvi dai chako!' Ni haki yetu binadamu kutendeana kwa heshima na kwa haki, lakini kila unapoamua sasa udai chako, basi ujue unatafuta ugomvi.
Sis tunalipa kodi kedekede katika nchi yetu. Lakini tunapoidai huduma bora, inakuwa ugomvi.

Hivi kwa nini? Mtanzania, eeh!