Monday, February 5, 2007

Kiswahili nacho kilitumika kuwakilisha.

Waalimu andamizi wa lugha toka nchini Tanzania wakiwakilisha kwa kutumia lugha ya kiswahili katika kongamano la walimu mbalimbali wa lugha lililofanyika San Diego huko Califonia. Toka kushoto ni Mwl. Juma Binagirioba (Bowling Green University) na Mwl. Zablon Mgonja (Fisk University).
Lugha ni chombo muhimu cha mawasiliano. Kama zilivyo lugha nyingine, kiswahili kwa sasa kinazidi kupata umaarufu si Afrika tu bali hata nje ya Afrika kama vile Amerika na Ulaya. Mathalani vyuo vingi nchini Marekani vimeanzisha idara za kiswahili ambapo wanafunzi wengi wanajiandikisha kwa ajili ya kujifunza lugha hii. Kama ilivyo kwa mlima Kilimanjaro, pia wamarekani wengi wanaamini ya kwamba kiswahili sanifu kinazungumzwa nchini Kenya. Kutokana na imani hiyo hata walimu wengi wanaofundisha kiswahili katika vyuo hivyo wanatoka nchini Kenya. Pamoja na hayo walimu wachache toka Tanzania wamepata umaarufu mkubwa na ufanisi wa hali ya juu kwa muda mfupi walioutumia kufundisha. Kimsingi katika bara la Afrika kiswahili sanifu kinazungumzwa nchini Tanzania. Tatizo hapa ni kwamba kuna mapungufu katika kuitangaza Tanzania yetu, lugha yetu ya kiswahili pamoja na vivutio lukuki tulivyonavyo. Kuna msemo usemao "usipozungumza hautajulikana kama upo" . Kwa msemo huu ni muda muhali sasa kuitangaza nchi yetu.

6 comments:

Anonymous said...

Mmh! makubwa sasa. Ina maana hao walimu wamegeuka kuwa wasanii au nimeelewa vibaya? Otherwise kiswahili kikizaniwa chaweza kuwa lugha ya bara la Afrika. Asante kwa hizi habari.

MICHUZI BLOG said...

mwalimu abou!

hongera kwa blogu nzuri yenye picha mwanana.kama ujuavyo picha yazungumza maneno alfu, kwa hiyo usiache kutoa ujumbe na picha. asante kwa kunitambulisha blogu yako hii. kaza buti

Unknown said...

je mtanzania aliyefudhu mafunzo ya lugha chuo kikuu akitaka kwenda kufundisha lugha ya kiswahili apitie njia zipi?hii ni opportunity nzuri kwa graduates wetu wanaozunguka mitaani bongo.

MTANZANIA. said...

Nawashukuruni nyote kwa kunitembelea.

Ni kweli kabisa anony. Hao walimu waliimba ule wimbo maarufu wa "Tanzania nakupenda" kwa kutumia kiswahili.

Michu ukiwa umebobea katika hii fani nakubaliana na wewe 100% kwamba picha moja yaweza kuwa na tafsiri 1000.

Zemarcopolo,kiunganishi pekee na muhimu kwa mtanzania aliyefuzu mafunzo ya lugha ni kupitia balozi mbalimbali za nchi husika zilizopo Tanzania. Kwa ubalozi wa Marekani kila mwaka mwezi wa 12 huwa wanatoa matangazo. Na watakaopitishwa watapangiwa vyuo vya kufundisha kwa muda wa mwaka moja. Kwa upande wa balozi nyingine kama vile Libya,Botswana n.k hawa wanatoa ajira za muda mrefu kwa walimu wa lugha toka Tanzania. Ni vizuri kuzitembelea balozi husika mara kwa mara.

Simon Kitururu said...

Natudumishe lugha yetu!Kiswahili Oyee!

Zablon Mgonja said...

Utamaduni wetu pia natuutangaze kwa nguvu kila tunapopata nafasi ya kufanya hivyo. Inasikitisha kwamba vijana wetu ( Wakiume) wa Tanzania wanasuka nywele na kujitoga kila sehemu ikiwa ni utamaduni uliosheheni sana huku Marekani.
Cha kushangaza wamarekani wengi wanadhani Afrika ni nchi moja na kwamba waafrika wote wnajuana,

JAmani kila ipatikanapo nafasi, tusilaze damu tuutangaze utamaduni wetu kwani ni fahari yetu. Tusiige tu kila kiiiiiiiiitu huku yetu mazuri tunayaficha