Friday, February 16, 2007

Wataiva lakini kwa mwezi moja?

Mh. Waziri mkuu ndugu Edward Lowasa.

Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari imefanikiwa kuanzisha shule nyingi za sekondari. Jambo hilo halikwenda sanjari na maandalizi ya walimu. Ili kukidhi matakwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Magreth Sitta amebainisha kuwa zaidi ya walimu 9000 wanahitajika. Tayari walimu 3,124 waliohitimu (mwezi mmoja) kabla ya muda wao wataajiriwa moja kwa moja na serikali pamoja na wengine 250 waliokuwa wamestaafu watarejeshwa kazini. Nafasi 6,000 zitajazwa na waliomaliza kidato cha sita ambao watapigwa msasa wa mafunzo ya ualimu kwa muda wa mwezi moja. Mwombaji anatakiwa awe na alama mbili za kufaulu mtihani wa kidato cha sita na baada ya mwezi moja atakuwa mwalimu wa sekondari. Inahitajika miujiza itakayomfanya muhitimu wa kidato cha sita kuwa mwalimu bora kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kimsingi kozi ya ualimu ina mambo mengi na inatakiwa isiwe pungufu ya miaka miwili. lngawa serikali inahitaji walimu wengi na kwa haraka, njia hii ina walakini kama kweli itatoa walimu bora au bora walimu.

11 comments:

Simon Kitururu said...

Hapa naona tutawapata bora walimu!Halafu hapo ndipo utashangaa kukuta wanafunzi hawajui wapaswayo kuyajua. Lakini vibosile hawana taabu.Watoto wao hawasomi kwenye shule hizi.

NDABULI said...

Simoni umesema kweli!
Hiki ni kiini macho, na wale wanasema ni wataalamu wa elimu wamekaa kimya, nadhani wale wanaosoma kuwa walimu kwa utaratibu ule wazamani wanahaki ya kudai wapewe vyeti haraka sana maana sioni mantiki yakuwa na walimu wa chapchap na wasio chapchap.
ndio mambo ya kupanga bila kufikiria hapo ni kama kumuuzia picha asiyeona.

Anonymous said...

Mi naogopa!! Hivi miaka 10 ijayo taifa litakuwa na kizazi cha aina gani katika suala zima la kufikiria na kuchambua mambo? Sijui.

Vempin Media Tanzania said...

kaka hatimaye nimetinga ndani ya jumba lako hongera kwa kutuhabarsha. Hakika hiki unachokisema ndo nilichokuwa na mashaka nacho mimi kwa kweli hawamadingi wanaipeleka nchi kuzimu

Simon Kitururu said...

Bro Abou eeh!Kwanini unahisi wataiva kwa mwezi mmoja tu?

Kibunango said...

Hii si mara ya kwanza, wakati ule wa UPE niliona kadhia kama hii, ingawa hii imezidi!

Simon Kitururu said...

@Mtanzania: usichukulie kwamba kwasababu nimesoma uliyoandika maanayake nimepata yote!Nahisi kunakitu hujasema bado katika topiki hii. Nakingojea!
Lakini nahisi tu!

MTANZANIA. said...

Kitururu! Kozi ya ualimu ina mambo mengi. Kuna mambo mengi ya kujifunza kwa nadharia kama vile saikolojia,mtaala,filosofia,nidhamu n.k. Baada ya hapo kuna mazoezi ya vitendo yaani practical teaching. Sasa kutokana na huo mtiririko wa mambo ndio maana nachelea kuona kama kweli mwezi moja utatosha kuwaivisha.

Kibunango! Sasa hii sijui tuiite USE (Universal Secondary Education)kama ilivyokuwa UPE enzi hizo.

MTANZANIA. said...

Asante kwa changamoto Kitururu.
Waweza nidokezea hicho nilichokisahau.
Mengi niliyoyaandika ni kutokana na mtazamo wangu kwani kitaaluma nami ni mwalimu na nilikaa chuoni miaka 4.

Simon Kitururu said...

@Mtanzania: katika comment zako mbili za hapo juu ulinijibu yale ambayo nilikuwa nahisi umeyaacha. Moja ni dondoo kwa mtazamo wako kama uliyepitia mafunzo ya ualimu, yale ambayo unauhakika hawa wa USE watayakosa. Unajua siye wengine ni rahisi kudakia hii hoja lakini kwasababu hatulijui kiundani inakuwa rahisi kusikia kwako kutokana nauzoefu wako katika taaluma na kama aliyepitia mfumo.
Mzee hapa kijiweni kwako mimi huwa sikosi.Lakini wakumlaumu kwa hilo ni wewe.

Anonymous said...

mie nimesoma ualimu kwa miaka sita!! yaani diploma miwili na degree minne!! na bado najiona nakosa baadhi ya mambo na hasa kusaidia wale slow learners halafu watukutu!
hapa ni mazingaombwe haya,inachosikitisha wanaofanya ivi ni educationists eg mama six!!!