Friday, February 9, 2007

Kama vile wanaimba "kama siyo juhudi zako Nyerere, CCM wangesoma wapiiii"


Wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu wakijumuika na wana-CCM wengine katika kusheherekea miaka 30 tangu kuzaliwa kwa chama hicho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Ni kama vile walijisahau na badala ya kusheherekea miaka 30 ya kuzaliwa kwa chama tawala (CCM), wanafunzi toka vyuo vya elimu ya juu walimtaka mwenyekiti wa chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. JK atoe msimamo wa serikali kuhusu wanafunzi wa taasisi hizo kuchangia 40% ya karo zao. Hakika majibu ya mheshimiwa Rais yalipokelewa kwa furaha pale aliposema serikali yake italiangalia upya suala hili. Kwa ujumla unapoongelea maendeleo ya taifa lolote hapa duniani ni nadra sana kutokuhusisha wasomi wa taifa hilo. Kimsingi wasomi kutoka taasisi za elimu ya juu ndio wataalamu wa kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kuchochea maendeleo. Kwa ufupi 40% kwa mtanzania mwenye kipato cha chini ni mzigo usiobebeka na kama hivyo ndivyo na msimamo wa serikali ukabaki kama ulivyo kuna uwezekano mkubwa kwa vijana wengi kushindwa kuendelea na masomo ya juu. Hii maana yake ni kwamba tabaka kati ya walio nacho na wale wasio nacho litazidi kuongezeka huku maendeleo ya nchi kwa ujumla yakizidi kudidimia. Ni vema suala hili likaangaliwa upya kama alivyosema kiongozi wa nchi. Elimu kama chachu ya maendeleo haina budi kutolewa bila vikwazo.

4 comments:

Anonymous said...

Nimekupata leo! Mimi naona huu ndiyo mfumo wa dunia ya sasa na si kila kitu lazima kifanywe na serikali. Lazima tujiulize "tunaifanyia nini serikali yetu?". Nitapita tena kesho kuona maoni mbalimbali.

Unknown said...

hawa vijana wanapewa label ya usomi lakini tabia zao hazijakaa kisomi.wananasa kwenye mitego rahisi sana,kuambiwa kuwa serikali ITALIFIKIRIA swala sio sababu ya kushangilia.pili,ni lazima watanzania tutoe mchango endelevu kwa taifa letu sio tu kufyonza kidogo kilichopo.hawa vijana na familia zao ni kweli kuwa wengi wao hawawezi kulipa hiyo pesa cash,lakini wakati wa likizo wengi wao huwa nyumbani tu bila shughuli maalum.mimi nilitarajia wasomi hawa waje na mawazo jinsi watavyokuwa wanafanya kazi za kujitolea wakati wa likizo na muda mwingine ambao hawana masomo ili kufidia gharama za kuwasomesha.kinyume chake,wasomi hawa wanalalamika wapewe msamaha wa deni na kinachofuata ni kwamba wakimaliza shule wanaingia kazini na kuanza tena kugoma kulalamikia mshahara mdogo,kama walivyofanya madaktari wetu pale muhimbili.sasa sisi tunategemea pesa za kuridhisha watu wabinafsi kiwango hiki zitoke wapi?????????

MTANZANIA. said...

Zemarcopolo nimekupata!
Kwa hiyo huu ni wakati wa "utaifanyia nini serikali na si serikali itakufanyia nini". Kukiwa na mipango thabiti bila shaka hili linawezekana.

Unknown said...

swadatah!