Kwa kasi hii Simba wa Teranga wajizatiti!!
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa stars) al-maarufu kama "JK boys" wakiwa mazoezini katika kituo cha mafunzo ya michezo cha Fluminense jijini Rio de Janeiro Brazil. Kutoka shoto ni Mwaikimba, Nsajigwa, Maulid & Yusuf. Picha na Benny Kisaka.
Katika dunia hii hakuna lisilowezekana. Waingereza wana msemo wao "nothing imposible under the sun" wakimaanisha hakuna kisichowezekana hapa duniani. Kama hivi ndivyo, bila shaka hakuna kitakachoishinda timu ya taifa ya kabumbu kufanya kile kinachosubiriwa kwa shauku kubwa na mamilioni ya wapenda kandanda kote nchini. Ikiwa inaongoza katika kundi lake, maendeleo ya timu si mabaya na kwa muda wa mwezi moja itakuwa nchini Brazil kwa ajili ya kujifua kabla ya kucheza na Senegal moja ya nchi zilizopata mafanikio makubwa katika mchezo wa mpira wa miguu barani Afrika. Lakini hicho si kikwazo cha kuifanya timu yetu iwe imefungwa hata kabla ya mchezo. Chini ya mwalimu Maximo toka Brazil nchi ambayo kiwango chake katika mchezo huu ni cha hali ya juu, wachezaji wote wanayapokea mafunzo yake vizuri na wanajituma katika kufanya mazoezi kama inavyotakiwa na tena kwa moyo mkunjufu. Serikali ilitoa tamko ya kwamba haitavumilia vitendo vya utovu wa nidhamu katika kambi hiyo na pia ni jukumu la wachezaji wote kuwa na moyo wa uzalendo. Kwa ufupi ni kwamba mtanange kati ya Stars na Simba wa Teranga itajumuisha wanaume 22 kwa uwiano wa wachezaji 11 toka kila upande. Haogopwi mtu hapa! si Diof, Camara wala Diop. Ni mabao tu toka kwa Mwaikimba, Maulidi na Maftah. Mungu ibariki Stars, Mungu ibariki Tanzania.
3 comments:
Naona vijana wamebadilika kwa muda mfupi waliokaa huko. Inatia matumaini na tuombe Mungu tutashinda.
duh...hawa jamaa wamejazia fresh hivyo.sasa hivi wanaonekana kama wale wachezaji wa cameroon.hawa jamaa watakuwa hatari sana!
Ni kweli wana miili inayotakiwa katika mikikimikiki ya mechi za kimataifa.
Zemarcopolo, hivi vitu vinawezekana kama kuna nia.
Post a Comment